IGAD yaichagua Taasisi ya chakula na lishe Tanzania kuwa kituo umahiri cha kikanda.

News Image

Imewekwa: 11th Nov, 2023

Wawakilishi na Wajumbe wa nchi zinazounda Mtandao wa Kujifunza juu ya ufuatiliaji wa Lishe (LENNS) unaoongozwa na IGAD, kwa pamoja wamekubaliana kuichaguaTaasisi ya Chakula na Lishe kuwa kituo cha umahiri cha Kikanda kitakachotumika katika kupanga, kupima. Kuchakata na kujenga uwezo wa vituo vingine katika taarifa za lishe zinazotokana na sampuli za vyakula na binadamu.

Wajumbe wa hao kutoka nchi za Ghana, Mali, Senegal, Djibouti, Malawi, Zambia, Rwanda, Kenya, Somalia pamoja na Uganda, walikuwa nchini Tanzania kushiriki kwenye Mkutano wa siku tatu wa kujadili namna ya kuimarisha mifumo ya takwimu za lishe katika nchi wanachama na namna nchi hizo zinavyoweza kushirikiana katika utekelezaji wa afua mbalimbali za kilishe.

Akifunga Kikao hicho kwa niaba ya Mkurugenzi wa IGAD Dkt. Girum Hailum, amesema utendaji kazi na uwekezaji uliofanywa na Serikali kwenye Taasisi na Maabara yake ya Chakula na Lishe iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam, vimepelekea kukubalika kuwa Kituo cha Umahiri cha kikanda ambacho nchi wanachama watakitumia kupanga, kupima, kuchakata na kujenga uwezo kwa vituo vingine hususani katika taarifa zinazotokana na Sampuli za vyakula na binadamu (damu na mkojo)

Wajumbe hao wamefikia hatua ya kuichagua Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania pamoja na Maabara yake iliyopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam, mara baada ya kufanikiwa kufika kwenye maabara hiyo na kujionea uwezo mkubwa ilionao katika kupima na kuchataka sampuli mbalimbali ya viashiria lishe kutoka nchi tofauti tofauti Afrika.