Hafla ya utiaji saini Mkataba wa usimamizi wa shughuli za lishe

News Image

Imewekwa: 30th Sep, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan atembelea banda la Maonyesho la Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania na kuagiza kupitiwa upya kwa Sera ya Lishe ya Mwaka 1992 kwa kuwa sera hiyo ni ya muda mrefu, hivyo inahitajika kufanyiwa mapitio ili kuendana na mabadiliko yaliyopo sasa.

Mhe.Samia Suluhu Hassan ni mgeni rasmi katika hafla ya utiaji saini Mkataba wa usimamizi wa shughuli za lishe, inayofanyika katika viwanja vya ukumbi wa Mikutano wa Jiji la Dodoma uliopo Mtumba. Hafla hii inafanyika kwa uratibu wa Ofisi ya Rais- TAMISEMI.