Fanyeni tafiti za kimkakati kuhusu masuala ya lishe

News Image

Imewekwa: 6th Dec, 2022

Na, Mwandishi wetu- Mara

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) Majaliwa amezitaka Taasisi zinafanya tafiti kuhusu masuala lishe, kufanya tafiti za kimkakati ili kusaidia Serikali kubaini hali ilivyo na kuchukua hatua stahiki za kisera na kiutendaji kwa wakati muafaka.

Akitoa agizo hilo na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalumu Mhe. Dkt. Doroth Gwajima kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kilele cha Mkutano mkuu wa nane wa wadau wa lishe nchini kilichofanyika Musoma mkoani Mara.

Waziri Gwajima amesema matokeo mazuri ya hali ya lishe yatapatikana kwa kufanya kazi kwa ushirikiano kupitia sekta mbalimbali na miradi inayotekelezwa kwa kuishirikisha jamii.

“kuna sababu nyingi za msingi zinazochangia hali duni ya lishe, ni ukweli usiofichika kuwa, ili kupata matokeo bora ya hali ya lishe, ni lazima tuhakikishe tunafanya kazi kwa pamoja na ushirikiano”. Alisema Mhe.Gwajima

Aidha Mhe.Gwajima amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo na ipo tayari kutoa kipaumbele katika kusaidia kutatua changamoto katika maeneo ambayo hayafanyi vizuri katika utekelezaji wa afua mbalimbali za kilishe.

Katika hatua nyingine Waziri Gwajima ameitaka OR-TAMISEMI kuhakikisha mikataba ya lishe kati ya Mheshimiwa Rais na Wakuu wa mikoa inaendelea kuboreshwa kwa kuingiza viashiria vitakavyosaidia kuongeza uwajibikaji katika sekta nyingine na kutoa taarifa.

MWISHO