21 Feb, 2026
Tarehe 12 Feb 2026, Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Mafunzo ya Lishe, Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Dkt. Esther Nkuba akitoa elimu ya lishe kwa wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule ya msingi Likwati manispaa ya Temeke ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Afya na Lishe unaotekelezwa katika shule za msingi 15 za Manispaa ya Temeke.
Afisa Mtafiti kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Eliasaph Mwana aelezea umuhimu wanafunzi kupata chakula shuleni kwa wazazi na walezi wa shule ya msingi Likwati ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Afya na Lishe unaotekelezwa katika shule za msingi 15 za Manispaa ya Temeke.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Likwati, Sosthenes Stephen Amasi aelezea namna Serikali yake itakavyohamasisha jamii kuchangia chakula cha watoto shuleni wakati wa kikao cha kuwaelezea wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule ya msingi Likwati umuhimu wa wanafunzi kupewa chakula shuleni ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Afya na Lishe unaotekelezwa katika shule za msingi 15 za Manispaa ya Temeke.
Mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano wa TFNC, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), na Manispaa ya Temeke
