Elimu ya Lishe Mitandaoni na Udhibiti Wake
10 May, 2026
Elimu ya Lishe Mitandaoni na Udhibiti Wake
Mei 8, 2026, Mkurugenzi Mtendaji wa TFNC, Dkt. Germana Leyna, ameshiriki katika kipindi cha asubuhi ndani ya Bongo FM (zamani TBC FM), akizungumzia mada muhimu ya “Elimu ya Lishe Mitandaoni na Udhibiti Wake.” Dkt. Leyna amesisitiza kuwa katika ulimwengu wa kidijitali, ni lazima wananchi wawe makini na taarifa za lishe wanazozipata. TFNC imeimarisha mikakati ya: 1.Kufuatilia na kukanusha taarifa potofu za lishe (Fact-checking). 2.Kutoa miongozo ya kisayansi kupitia majukwaa ya kijamii. 3.Kushirikiana na mamlaka za udhibiti kulinda afya ya mlaji. Lishe Bora ni Msingi wa Maendeleo.