10 May, 2026
Mei 6, 2026, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amezindua tafiti mbili za kimkakati:
1.Uwezeshaji wa Wanawake na Lishe (2023/24)
2.Jinsia na Mazingira (2025)
Katika hafla hiyo, Mhe. Waziri amemkabidhi nakala za matokeo hayo Afisa Lishe Mwandamizi kutoka TFNC, Bi. Maria Ngilisho ambaye alikuwa miongoni wageni waalikwa walioshiriki katika uzinduzi huo.
Takwimu hizi ni muhimu,Zitasaidia Serikali na wadau kupanga mipango yenye tija katika kuimarisha lishe ya jamii, kutetea usawa wa kijinsia, na kukabiliana na mabadiliko ya mazingira kwa uhakika zaidi.
Takwimu sahihi ni msingi wa maendeleo!
