Dkt. Yonazi aongoza kikao cha wadau wa lishe kuelekea maandalizi ya mkutano mkuu wa wadau wa lishe nchini.

Imewekwa: 25th May, 2024
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt.Jim Yonazi leo Mei 24 2024, ameongoza kikao cha Wadau wa lishe cha mashauriano ya maandalizi ya Mkutano mkuu wa wadau wa lishe nchini, na maandalizi ya kupitia muda wa pili wa utekelezaji wa Mpango wa Pili Jumuishi wa Taifa wa Masuala ya Lishe (NMNAP II).
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi za Waziri Mkuu zilizopo Magogoni jijini Dar es Salaam na kuhusisha wadau kutoka mashirika na Taasisi mbalimbali, Dkt.Yonazi amewapongeza na kuwashukuru kwa kujitoa kwao katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za lishe nchini, na kuwaomba kuendelea kushirikiana na Serikali.