Ugeni wa Maafisa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF)

News Image

Imewekwa: 14th Jun, 2022

Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania June 13, 2022 imetembelewa na Maafisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) kutoka Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini Mwa Afrika ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hiyo katika kukabiliana na matatizo mbalimbali ya kilishe Nchini.

Maafisa hao waliongozana na Msimamizi Mkuu wa Shughuli za lishe nchini kutoka Shirika hilo Bw. Patrick Codjie walifanikiwa kutembelea maabara ya Taasisi ya Chakula na Lishe na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika katika maabara hiyo ikiwemo za upimaji wa virutubishi mbalimbali katika vyakula.

Tanzania Census 2022