UFUNGAJI WA MAFUNZO YA WASHIRIKI UTAFITI WA AFYA YA MAMA NA MTOTO NA VIASHIRIA VYA MALARIA WA MWAKA 2021-2022

News Image

Imewekwa: 23rd Feb, 2022

Naibu waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel amefunga mafunzo ya washiriki wa Utafiti wa Afya ya Mama na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa mwaka 2021-2022 na kuwataka washiriki wa utafiti huo kukusanya taarifa za utafiti kwa weledi ili Taifa lipate takwimu rasmi za afya zitakazosaidia katika upangaji na utekelezaji wa sera.

Katika Utafiti huo Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania inatoa ushauri wa Kitaalamu na kuratibu utafiti huo pamoja na maabara yake ya Chakula itatumika kufanya vipimo vyote vya viashiria lishe baada sampuli kukusanywa.