Ufuatiliaji wa Zoezi la Upimaji Afya na Lishe shuleni - Zanzibar

Imewekwa: 8th Feb, 2022
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt Germana Leyna akiwa katika ufuatiliaji wa zoezi la Upimaji afya na lishe shuleni kwa ajili ya Utafiti unaofanywa na Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Zanzibar kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali pamoja na Ofisi ya Takwimu Zanzibar ambapo katika Utafiti huu Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania ni washauri wa utekelezaji wa utafiti, ambao unafadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF).