TFNC YASHIRIKI MJADALA WA KUIMARISHA HUDUMA ZA LISHE KATIKA MIFUMO YA AFYA YA MSINGI KUPITIA MKUTANO WA PILI WA KIMATAIFA WA HUDUMA ZA AFYA YA MSINGI (IPHCC- 2026)
11 Sep, 2026
TFNC YASHIRIKI MJADALA WA KUIMARISHA HUDUMA ZA LISHE KATIKA MIFUMO YA AFYA YA MSINGI KUPITIA MKUTANO WA PILI WA KIMATAIFA WA HUDUMA ZA AFYA YA MSINGI (IPHCC- 2026)
  ARUSHA: Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) imeshiriki katika Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Huduma za Afya ya Msingi (IPHCC2026) uliofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 9 Septemba, 2026 mpaka 11 septemba 2026 Mkutano huo muhimu umewakutanisha wataalamu na wadau mbalimbali kutoka sekta za afya, lishe na mazingira kutoka mataifa 26  ya Africa, Asia, Ulaya na America na wadau wengine kutoka Tanzania, Eswatini, Angola, WHO AFRO, CDC Africa na ECSA-HC ili kujadili namna ya kuimarisha upatikanaji wa huduma za Afya ya msingi pamoja na huduma za lishe. Katika Mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Dkt. Germana Leyna  ameongoza mjadala (Moderator) uliowakutanisha wataalamu mbalimbali kujadili uzoefu, changamoto na fursa katika kuimarisha huduma za lishe kupitia mfumo wa afya ya msingi  Aidha umuhimu wa kuunganisha sera, mipango na utekelezaji wa afua za lishe katika ngazi mbalimbali ili kuongeza ufanisi na upatikanaji wa huduma za lishe kwa wananchi hususan kwa wanawake, watoto, vijana na familia katika ngazi za jamii na vituo vya kutolea huduma ulisisitizwa. Mkutano huo ambao umegitimishwa leo, 11 Septemba 2026, umetoa fursa kwa Tanzania, Afrika na jumuiya ya kimataifa kutafakari hatua zilizofikiwa katika utoaji wa huduma za Afya ngazi ya msingi na kuweka mikakati ya pamoja ya kuhakikisha hakuna mtu anayeachwa nyuma.