25 Jan, 2026
Tarehe 16 Januari 2026, watafiti kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Baadhi wa Wanafunzi wa Shahada za Juu za Epidemiolojia ya Lishe pamoja na Sayansi ya Lishe kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), wameshiriki semina inayohusu uhusiana baina ya Kilimo, Lishe na Afya ( Agriculture Nutrition and Health (ANH) Linkages)
Semina hiyo ililenga kuwajengea uwezo watafiti hao namna ya kupambana na changamoto za utapiamlo kwa kutumia taaluma zaidi ya moja kwa mara pamoja, ambazo ni taaluma za Kilimo, Lishe na Afya.Semina hiyo ya uhusiano baina ya Kilimo, Lishe na Afya ilifunguliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) na iliwasilishwa na Watalamu ambao ni Wanafunzi wa Shahada za Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ambao ni Eward Mushi, Mtaalam wa Uchumi Kilimo na Victoria Kariathi, Mtaalam wa Lishe ya Binadamu.
