Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Mifugo (Nanenane) yanaendelea Jijini Dodoma

News Image

Imewekwa: 6th Aug, 2024

Tunaendelea na utoaji elimu wa masuala ya Chakula na Lishe katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Mifugo (Nanenane) yanayofanyika katika uwanja wa Nzuguni jijini Dodoma.


Mkurugenzi Mtendaji wa wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Frank Nyabundege (wa pili kulia) akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT Geofrey Kirenga, wametembelea banda la maonesho la TFNC liliopo katika Viwanja vya Nanenane Nzunguni Dodoma, na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi katika utekelezaji wa Afua mbalimbali za lishe nchini.

Mbunge wa Viti Maalum kutokea Mkoa wa Mbeya Mhe. Sophia Mwakagenda(picha kulia), akijiandikisha katika kitabu cha Wageni cha Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, mara baada ya kutembelea banda la Taasisi katika Maonesho ya kimataifa ya Kilimo na Ufugaji Nanenane yanayoendelea kufanyika katika Viwanja Vya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma.

Mhe.Mwakagenda alipata fursa ya kufahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi na namna inavyoshirikiana na wadau katika utekelezaji wa afua mbalimbali za kilishe.
Karibuni sana katika banda la maonesho la Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania

Viongozi wa Wakulima(picha ya kushoto) wa kijiji cha Nyororo kilichopo Mafinga mkoani Iringa, wakipokea elimu ya lishe na namna ya kuandaa mlo kamili kwa kutumia vyakula vinavyopatikana katika maeneo yao, mara baada ya wakulima hao kutembelea banda la Taasisi ya Chakula na Lishe katika maonesho ya kimataifa ya kilimo na ufugaji nanenane yaliyopo katika viwanja vya Nanenane Nzuguni jijini Dodoma

Karibuni sana katika banda la maonesho la Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania