Maafisa lishe wahimizwa kuwa wabunifu katika kufanya tafiti maeneo ya tiba lishe na afya ya jamii

News Image

Imewekwa: 6th Apr, 2022

Na Jackson Monela

Maofisa Lishe nchini wametakiwa kuwa wabunifu katika kufanya tafiti kwenye maeneo ya tiba lishe na afya ya jamii kwa ujumla ili kuleta manufaa nchini

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mafunzo na Elimu ya Lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe nchini Dkt. Esther Nkuba wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa chama cha Wanataaluma wa Lishe Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam

Dkt. Nkuba amesema ni lazima wawe wabunifu ili chama chao kionekane bora kwa kuibua mambo ya msingi ambayo yatakayo leta tija katika Taifa.

"Inabidi tujisimamie, ni lazima tuwe wabunifu ili chama chetu kionekane kwa kuibua mambo ya msingi ambayo yataleta tija katika taifa letu"amesema Dkt. Nkuba

Aidha, Dkt. Nkuba amewaasa Maafisa lishe kuhakikisha huduma za lishe zinazotelewa nchini ziwe na ubora wa na kuzingatia maadili ili kuleta tija kwa wagonjwa

"Hakikisheni huduma za lishe zinatolewa kwa ubora wa hali ya juu na kwa kuzingatia maadili ya taaluma zenu "amesema Dkt. Nkuba

Hata hivyo Dkt. Nkuba amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mbele katika kujitoa kupambana na utapiamlo nchini na kuhakikisha lishe inaenda vizuri katika nchi yetu,

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa huduma za lishe kutoka Wizara ya Afya Bi. Grace Moshi amewataka maafisa hao kufanya kazi kwa kujitoa na yenye ubora wa hali ya juu kama anavyo himiza Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu.

"Naomba tujisimamie, tuhakikishe tunatoa huduma bora za tibalishe na afya ya jamii kwa ujumla katika vituo vyetu ili kuhakikisha vina simama sawasawa "amesema Grace Moshi.

Tanzania Census 2022