Maadhimisho Wiki ya Unyonyeshaji Maziwa ya Mama 1-7 Agosti, 2024

News Image

Imewekwa: 3rd Aug, 2024

Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) imeendelea kutoa elimu ya lishe bora kwa akina mama wanaonyonyesha ili kumwezesha mama kuwa na maziwa ya kutosha kwa ajili ya Mtoto wake.

Pichani ni Afisa Lishe Mtafiti Mwandamizi Maria Ngilisho (aliyesimama) akitoa elimu kwa akina mama wanaonyonyesha ikiwa ni mwendelezo wa utoaji elimu ya unyonyeshaji katika jamii katika kipindi hiki cha Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Maziwa ya Mama Duniani.