Elimu ya lishe inaendelea kutolewa

News Image

Imewekwa: 12th Jun, 2024

Afisa Lishe Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Bi.Maria Ngilisho, akiendelea kutoa elimu ya Lishe kwa wakazi waliokuwa wakielekea Mbagala ikiwa ni Mwendelezo wa “Kampeni ya Lishe Bora kwa Njia ya Daladala” ambayo imelenga kuongeza uelewa kwa wanajamii juu ya matumizi sahihi ya Chakula na kuhamasisha ulaji unaofaa kwa kila mmoja wetu ili kuweza kupunguza matatizo ya kilishe miongoni mwa Watanzania.

Ukiwa ndani ya Daladala hii elimu utakayopatiwa itazingatia Mwongozo wa Taifa wa Chakula na Ulaji Sahihi ambao umezingatia uwepo na matumizi ya vyakula vya asili vilivyopo katika mazingira yetu, na kuelekeza vipimo sahihi kwa kila mlo au chakula na kinywaji ambacho binadamu anatakiwa kupata kwa siku.