Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji wa Maziwa ya Mama huadhimishwa kila mwaka kwa lengo la kuhamasisha jamii kushiriki ipasavyo katika kufanikisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema "Thamini Unyonyeshaji; weka mazingira wezeshi kwa mama na mtoto".