Wawakilishi mradi wa LEG4DEV watembelea TFNC na kufanya mazungumzo

News Image

Imewekwa: 29th Mar, 2023

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna( mwenye koti jekundu) amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa mradi wa LEG4DEV (Scaling Legume for Development) unaotekelezwa katika nchi za Zambia, Malawi, Tanzania na Ethiopia ukilenga kufanya shughuli za Utafiti utakaosaidia kuongeza kiwango cha ulaji wa mazao ya Mikunde katika nchi hizo.

Mradi wa LEG4DEV unafadhiliwa na Shirila la Umoja Ulaya na utekelezaji wake unafanyika kwa kuongozwa na Chuo Kikuu cha Galway cha nchini Ireland, huku ukishirikisha mashirika mengine ya IITA, CIMMYT pamoja na ILRI.