Mafunzo ya Usindikaji Unga Mchanganyiko kwa matumizi ya Watoto wenye umri wa miezi 6-23
Mafunzo ya Usindikaji Unga Mchanganyiko kwa matumizi ya Watoto wenye umri wa miezi 6-23
21 Apr, 2026
USAJILI : BONYEZA HAPA KUJISAJILI
Mada zitakazofundishwa:
- Masuala ya msingi kuhusu chakula cha nyongeza kwa watoto
- Uongezaji wa virutubishi kwenye vyakula Tanzania
- Kanuni bora za usindikaji wakati wa kuandaa unga mchanganyiko:
- Mbinu za kupunguza sumu kuvu
- Mbinu za kuzuia vimelea vya magonjwa
- Hatua za usindikaji wa unga mchanganyiko kwa kutumia mazao ya kawaida na yaliyoongezwa virutubishi kibailogia
- Aina za michanganyiko ya unga
Walengwa wa mafunzo: Wajasiliamali wanaosindika vyakula vya watoto wenye umri wa miezi 6 hadi 23.
Sifa za mwombaji: Awe na uwezo wa kusoma na kuandika
Lugha ya mafunzo: Kiswahili
Tarehe: 22–24 Mei 2026
Mahali: TFNC – Mikocheni (Mtaa wa Sembeti)
Ada: TZS 160,000
(Inajumuisha chakula, ukumbi na cheti)
